Jinsi ya kutengeneza ndizi za mzuzu na nazi ya kupaka

Asalaam aleikum warahmatullah wabarakatu, natumai swaum zinaendelea salama. Safari hii nimechelewa kupost mapishi ya iftar, kuna baadhi ya mapishi nataka nijaribu, nikiyapatia vizuri In shaa Allah nizipost. Ila kwa sasa hivi ntapost marudio ya mapishi ya ramadhani ya mwaka jana.

Mwenyezimungu abariki funga zetu na apokee swaum zetu. Ramadhan njema.

Mahitaji

  • Ndizi mzuzu kilo moja
  • Nazi 400ml
  • Maji 400ml
  • Iliki

Maandalizi

  • Menya, kata ndizi zako
  • Weka ndizi, nazi 200ml, maji 400ml na iliki kwenye sufuria, kisha bandika jikoni viive.
  • Angalia zisiive sana kiasi cha kumong’onyoka. Zikisha iva, zima jiko.

Jinsi ya kutengeneza tui la kupaka

Mahitaji

  • Nazi 200ml
  • Ngano kijiko kidogo nusu (hii unatumia kama tui lako ni jepesi mno)


Maandalizi

  • Chemsha tui lako kwenye kisufuria kidogo. Likianza kuchemka, koroga taratibu hadi liive ili tui lisikatike.
  • Tui lako litakuwa tayari kama likiwa zito na linatoa mapovu wakati likichemka.
  • Ikiwa tui lako ni jepesi na haliwi zito, changanya ngano na maji vijiko vikubwa vitatu, kisha mimina taratibu kwenye tui lako. Usimimine lote kwa wakati mmoja, likianza kuwa zito, acha lichemke mpk liive.
  • Changanya tui lako na ndizi kwa kutumia kijiko. Fanya hivi taratibu kuepusha ndizi kumong’onyoka.
  • Ndizi zako tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kutengeneza sambusa

Mahitaji

  • Nyama ya kusaga 1kg
  • Viungo (2tsp turmeric, 1 tbsp ginger powder, 2tbsp paprika powder, 2tbsp curry powder, 2tbsp meat flavour stock)
  • Vitunguu 2-3 vikubwa
  • Hoho 1
  • Thomu iliyosagwa 2tbsp
  • Carrot zilizokwanguliwa 250mg (grated carrots)
  • Manda za sambusa (spring roll pastry)
  • Mafuta ya kukaangia
  • parsley/coriander (dania)
  • Limau 2-3
  • Ngano ya kufungia manda

Jinsi ya kutengeneza

  • Weka mchanyiko wa nyama, viungo, thomu, juice ya limau  kwenye sufuria kubwa. Kisha bandika jikoni.
  • Kataka vitunguu, dania na hoho vipande vidogovidogo na vyembamba. Kisha visafishe, bila kusahau carrot zako. Zichuje vizuri.
  • Usisahau kuigeuza nyama yako. Onja kama imeiva
  • Mimina mchanganyiko wa vitunguu kwenye nyama. Acha ichemke kwa dakika 5-10, kisha onja kama chumvi na viungo vipo sawa. Kama ndogo ongeza. kisha acha ichemke mpaka ukavu maji. Hakikisha imekauka. Kisha zima jiko. Acha ipoe
  • Weka ngano kwenye kibakuli, weka maji, koroga ilikupata mchanganyiko *gundi*
  • Funga manda zako, jaza sambusa. Bonyeza link hapo chini kama hujui jinsi ya kufunga sambusa.
  • Choma sambusa zako. Tayari Kula.
  • Unaweza kuchoma zote au ukahifadhi baadhi kwenye freezer.

How to fold Samosa (2 Ways) By Rubina Asif – YouTube

Jinsi ya kutengeneza mahamri

Mahitaji

  • Ngano 1kg
  • Sukari robo (kama weye ni mpenzi wa sukari, unaweza ukaongeza)
  • Hamira packet 2 za 7g
  • Bakingpowder paket 1 ya 7g
  • Nazi au maziwa 1ltr
  • Iliki iiyosagwa 2tbs
  • Mayai 3
  • Mafuta ya kupikia 1ltr
  • Makuli kubwa la kukandia
  • Karai
  • Kibao na msukumio

Maandalizi

  • Mimina mafuta kidogo au samli (150ml) kwenye kisufuria kidogo, kisha iweke jikoni yapate moto.
  • Mimina unga, sukari na iliki kwenye bakuli la kukandia, kisha vichanganye vizuri
  • Mafuta yakishapata moto vizuri mimina kwenye mcchanganyiko wa unga, angalia usiungue.
  • Changanya mafuta na unga vizuri, kisha weka hamira na bakingpowder. Changanya vizuri
  • Vunja mayai na changanya kwenye mchanganyiko wa unga.
  • Mimina nazi au maziwa ya uvuguuvugu taratibu kwenye unga, mpaka upate donge moja. Mchanganyiko usiwe mgumu sana na usiwe chapachapa.
  • Kanda ngano yako hadi iumuke.
  • Kata madonge tisa. Sukuma kisha kata.
  • Bandika Karai lako, weka mafuta, anza kuchoma mahamri yako.
  • Yakiwa rangi ya brown, yatoe.
  • Mahamri yako tayari kuliwa.

Unaweza kula na mbaazi, maharage au mchuzi.

Eid Mubarak

Nawatakia Eid njema kwa waisilamu wote, iwe unasherekea siku ya leo au kesho. Mwenyezimungu apokee funga zetu na atujaalie uhai tuione ramadhani nyengine, Ameen InShaa Allah. Kwa walioshindwa kufunga ramadhani hii, In Shaa Allah kheri mwakani panapo majaaliwa.

Eid Mubarak

Jinsi ya kutengeneza mahamri

Mahitaji

  • Ngano 1kg
  • Sukari robo (kama weye ni mpenzi wa sukari, unaweza ukaongeza)
  • Hamira packet 2 za 7g
  • Bakingpowder paket 1 ya 7g
  • Nazi au maziwa 1ltr
  • Iliki iiyosagwa 2tbs
  • Mayai 3
  • Mafuta ya kupikia 1ltr
  • Makuli kubwa la kukandia
  • Karai
  • Kibao na msukumio

Maandalizi

  • Mimina mafuta kidogo au samli (150ml) kwenye kisufuria kidogo, kisha iweke jikoni yapate moto.
  • Mimina unga, sukari na iliki kwenye bakuli la kukandia, kisha vichanganye vizuri
  • Mafuta yakishapata moto vizuri mimina kwenye mcchanganyiko wa unga, angalia usiungue.
  • Changanya mafuta na unga vizuri, kisha weka hamira na bakingpowder. Changanya vizuri
  • Vunja mayai na changanya kwenye mchanganyiko wa unga.
  • Mimina nazi au maziwa ya uvuguuvugu taratibu kwenye unga, mpaka upate donge moja. Mchanganyiko usiwe mgumu sana na usiwe chapachapa.
  • Kanda ngano yako hadi iumuke.
  • Kata madonge tisa. Sukuma kisha kata.
  • Bandika Karai lako, weka mafuta, anza kuchoma mahamri yako.
  • Yakiwa rangi ya brown, yatoe.
  • Mahamri yako tayari kuliwa.

Unaweza kula na mbaazi, maharage au mchuzi.

Jinsi ya kutengeneza vitumbua

Mahitaji

  • Mchele vikombe viwili (nusu kilo) loweka usiku kucha
  • Tui vikombe viwili
  • Sukari kikombe kimoja
  • Hamira packet moja (kijiko kimoja)
  • Iliki kijiko kimoja cha chai
  • Mayai mawili
  • Mafuta ya kupikia

Maandalizi

  • Kikombe utakachotumia kupimia mchele, ndicho utakachopimia sukari na tui.
  • Chuja mchele uloloweka vizuri, hakikisha hamna maji yamebakia
  • Mimina tui, mchele, sukari, iliki na hamira kwenye blender, chanya mchanganyiki kwa kutumia kijiko ili iwe sawa kisha washa blender lako.
  • Saga kwa takriban dakika 10, pumzisha blender lako kila baada ya dakika 2- 3 hii ni kuepusha blender lako lisiungue. Saga hadi uwe laini.
  • Angalia uzito ulivyo, kama mzito sana ongeza tui kidogo.
  • Weka mchanganyiko wako kwenye bakuli, ufunike na kisha uweke kwenye sehemu yenye joto uumuke . Unaweza uacha uumuke kwa lisaa limoja au mawili au ukiuona ujazo umekuwa marambili yake.
  • Baada ya kuumuka weka mayai mawili, kisha changanya mchanganyiko wako vizuri kwa kutumia upawa.
  • Bandika kikaangio chako cha vitumbua jikoni na mchanganyiko upo tayari kwa kuchoma.

Enjoy!!!!!

Pepper beef stir

Ingredients :

For the marination:

  • Tender meat – 1kg
  • White Pepper powder- 1 tsp
  • Ginger garlic paste – 3 tbsp
  • Meat stock flavour – 1 tbsp
  • Egg – 1

For the coating:

  • Cornflour- 1 cup

For Tempering:

  • Ginger garlic paste – 3tbsp

Other Ingredients:

  • Green bell pepper, diced – 2
  • Red bell pepper, diced- 1
  • Yellow bell pepper, diced – 1
  • Orange bell pepper, diced – 1
  • Red onions, sliced- 2
  • Soy sauce- 1/4 cup
  • Tomato Ketchup- 4 tbsp
  • Vinegar- 2 tsp
  • Black Pepper Powder- 1 tsp
  • Garlic powder – 1 tsp
  • Meat spice – 1 tsp
  • Ras El Hanout
  • Paprika powder
  • Cornflour slurry- 1/2 cup cornflour mixed in 150ml water
  • Oil- 4 tbsp
  • Spring Onion greens, chopped, for garnish- 1 cup
  • Parsley, chopped for garnish – 1 cup

Preparation:

  • Wash and cut the meat pieces into 1” pieces
  • Marinate with the items indicated. Mix well and set aside for 30 mins – 1hr.
  • After 30mins – 1hr, mix in the corn flour to coat the meat pieces.
  • Dice the onion, green, yellow, orange and red pepper.
  • Slice the red onions and chop the greens + parsley for garnish.

Proces

  • To fry the meat pieces, heat oil till medium hot and drop the battered meat pieces one at a time. Do not crowd the pan and if required, fry in batches.
  • Fry on medium heat for 5-6 mins till golden. Remove and keep on a plate.
  • Now take a wok or a pot & heat 4 tbsp oil.
  • Add the ginger garlic paste and stir for 15 secs.
  • Now add the diced red onions, mix and fry on high heat for a minute.
  • Add the green, yellow, orange and red peppers,mix & stir fry the vegetables on high heat for a minute.
  • Now add the soy sauce, tomato ketchup, mix & stir fry on high heat for 15 secs.
  • Add the vinegar & black pepper powder, ginger powder, paprika powder, meat spice, ras el hanout & stir fry on high heat for 15 secs, add a splash of water if required.
  • Add the fried meat pieces and mix & stir fry on high heat for 1 min till these are coated by the sauce.
  • Add the corn slurry, mix & stir fry cook for 30 secs.
  • Garnish with spring onion greens,parsley, mix and serve .

CHICKEN MANCHURIAN | RESTAURANT STYLE CHICKEN MANCHURIAN RECIPE – YouTube