Vipimo
Mchele (Basmati) 3 vikombe
Nyama ya ngo’mbe 1 kg
Pilipili boga 1 kubwa
Nyanya 2 kubwa
Vitunguu maji 2 vikubwa
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Tangawizi 1 kijiko cha chai
Ndimu 1
Mafuta ya kupikia ½ kikombe
Mdalasini ½ kijiko cha chai
Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ½ Kijiko cha chai
Hiliki ½ Kijiko cha chai
Namna ya kutayarisha na Kupika
- Roweka mchele wako katika chombo
- Chukuwa nyama na ioshe vizuri na itie thomu, tangawizi, ndimu, pilipili manga na chumvi kiasi
- Iweke jikoni hadi ikauke maji na kuwa imewiva huku ukiikaanga kaanga kwa hayo hayo mafuta yake hadi kuwa rangi ya hudhurungi
- katakata Vitunguu na nyanya weka pembeni
- Chukua pilipili boga, thomu, tangawizi na visage katika mashine ya kusagia
- Weka sufuria pembeni na utie mafuta, subiri yapate moto
- Kisha tia vitunguu na vikaange hadi kuwa hudhurungi na tia nyanya
- Kisha mimina mchanganyiko wako ulio usaga wa pilipili boga, thomu na tangawizi
- Koroga kwa dakika kadhaa Kisha mininia nyama uliyokuwa tayari, maji kiasi na chumvi wastani na subiri maji hayo yachemke
- Weka mchele humo na koroga kiasi na onja chumvi kama ipo sawa au kama ndogo unaweza kuongeza
- Funika na punguza moto na uache uive taratibu
- Baada ya kukauka maji kabisa basi ugeuze na subiri tena kwa dakika kama mbili na tayari kuliwa.