Wali wa carrot na kuku wakukaanga

Vipimo Vya Wali
– Mchele wa Basmati/Pishori – 1 kilo moja
– Vitunguu maji – 3
– Karoti – 2
– Siagi – 3 vijiko vya supu
– Kidonge cha supu (stock) – 1 kimoja
– -Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
– Osha mchele uroweke kama saa moja au mbili
– Katakata vitunguu vipande vidogodogo (chopped) weka kando.
– Kwaruza karoti (grate) weka kando.
– Tia siagi katika sufuria ya kupikia wali, weka katika moto iyayuke
– Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kiasi tu.
– Tia maji kiasi ya kupikia wali, changanya na kidonge cha supu.
– Yakichemka tia mchele, koroga, funika uweke moto mdogo mdogo.
– Kabla ya maji kukauka tia karoti changanya wali kisha funika uive kama unavyopika pilau.

Vipimo Vya Kuku Wa Kukaanga
– Kuku alokatwakatwa – 1
– Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa – 2 vijiko vya supu
– Bizari ya mchanganyiko/garam masala – kijiko cha supu
– Mtindi/Yoghurt – 1 kijiko cha supu
– Ndimu – 1
– Chumvi – kiasi
– Mafuta ya kukaangia – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
– Ukishamuosha kuku, mchuje atoke maji yote.
– Changanya viungo vyote katika kibakuli kidogo.
– Changanya pamoja na kuku kisha acha akolee viungo (marinate) kwa muda wa masaa  mawili takriban.
– Weka mafuta katika karai na kaanga kuku, akiwiva yu tayari kuliwa na wali.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s