Mahitaji
- Nyama ya kusaga 1kg
- Viungo (2tsp turmeric, 1 tbsp ginger powder, 2tbsp paprika powder, 2tbsp curry powder, 2tbsp meat flavour stock)
- Vitunguu 2-3 vikubwa
- Hoho 1
- Thomu iliyosagwa 2tbsp
- Carrot zilizokwanguliwa 250mg (grated carrots)
- Manda za sambusa (spring roll pastry)
- Mafuta ya kukaangia
- parsley/coriander (dania)
- Limau 2-3
- Ngano ya kufungia manda
Jinsi ya kutengeneza
- Weka mchanyiko wa nyama, viungo, thomu, juice ya limau kwenye sufuria kubwa. Kisha bandika jikoni.
- Kataka vitunguu, dania na hoho vipande vidogovidogo na vyembamba. Kisha visafishe, bila kusahau carrot zako. Zichuje vizuri.
- Usisahau kuigeuza nyama yako. Onja km imeiva
- Mimina mchanganyiko wa vitunguu kwenye nyama. Acha ichemke kwa dakika 5-10, kisha onja kama chumvi na viungo vipo sawa. Kama ndogo ongeza. kisha acha ichemke mpaka ukavu maji. Hakikisha imekauka. Kisha zima jiko. Acha ipoe
- Weka ngano kwenye kibakuli, weka maji, koroga ilikupata mchanganyiko *gundi*
- Funga manda zako, jaza sambusa. Bonyeza link hapo chini kama hujui jinsi ya kufunga sambusa.
- Linka ya YouTube — https://www.youtube.com/watch?v=TR9F993TiM4
- Choma sambusa zako. Tayari Kula.
- Unaweza kuchoma zote au ukahifadhi baadhi kwenye freezer.
Baadhi ya spices nlizotumia mie. Unaweza tumia unazopenda weye mwenyewe.
Carrot unaweza nunua zima, kisha ukazikwangua mwenyewe nyumbani. Mie nanunuaga zilizo kwanguliwa tayari.
Pia unaweza tumia nyama ya kusanga ya kuku, binafsi napenda sambusa za nyama ya kusaga ya ng’ombe.
Unaweza kutengeneza manda zako mwenyewe.
Kuna wanaotumia mayai badala ya ngano kufungia sambusa zao.
You must be logged in to post a comment.