
Mahitaji
- Nyama ya kusaga 1kg
- Viungo (2tsp turmeric, 1 tbsp ginger powder, 2tbsp paprika powder, 2tbsp curry powder, 2tbsp meat flavour stock)
- Vitunguu 2-3 vikubwa
- Hoho 1
- Thomu iliyosagwa 2tbsp
- Carrot zilizokwanguliwa 250mg (grated carrots)
- Manda za sambusa (spring roll pastry)
- Mafuta ya kukaangia
- parsley/coriander (dania)
- Limau 2-3
- Ngano ya kufungia manda
Jinsi ya kutengeneza
- Weka mchanyiko wa nyama, viungo, thomu, juice ya limau kwenye sufuria kubwa. Kisha bandika jikoni.
- Kataka vitunguu, dania na hoho vipande vidogovidogo na vyembamba. Kisha visafishe, bila kusahau carrot zako. Zichuje vizuri.
- Usisahau kuigeuza nyama yako. Onja km imeiva
- Mimina mchanganyiko wa vitunguu kwenye nyama. Acha ichemke kwa dakika 5-10, kisha onja kama chumvi na viungo vipo sawa. Kama ndogo ongeza. kisha acha ichemke mpaka ukavu maji. Hakikisha imekauka. Kisha zima jiko. Acha ipoe
- Weka ngano kwenye kibakuli, weka maji, koroga ilikupata mchanganyiko *gundi*
- Funga manda zako, jaza sambusa. Bonyeza link hapo chini kama hujui jinsi ya kufunga sambusa.
- Choma sambusa zako. Tayari Kula.
- Unaweza kuchoma zote au ukahifadhi baadhi kwenye freezer.