Jinsi ya kutengeneza vitumbua

Mahitaji

  • Mchele vikombe viwili (nusu kilo) loweka usiku kucha
  • Tui vikombe viwili
  • Sukari kikombe kimoja
  • Hamira packet moja (kijiko kimoja)
  • Iliki kijiko kimoja cha chai
  • Mayai mawili
  • Mafuta ya kupikia

Maandalizi

  • Kikombe utakachotumia kupimia mchele, ndicho utakachopimia sukari na tui.
  • Chuja mchele uloloweka vizuri, hakikisha hamna maji yamebakia
  • Mimina tui, mchele, sukari, iliki na hamira kwenye blender, chanya mchanganyiki kwa kutumia kijiko ili iwe sawa kisha washa blender lako.
  • Saga kwa takriban dakika 10, pumzisha blender lako kila baada ya dakika 2- 3 hii ni kuepusha blender lako lisiungue. Saga hadi uwe laini.
  • Angalia uzito ulivyo, kama mzito sana ongeza tui kidogo.
  • Weka mchanganyiko wako kwenye bakuli, ufunike na kisha uweke kwenye sehemu yenye joto uumuke . Unaweza uacha uumuke kwa lisaa limoja au mawili au ukiuona ujazo umekuwa marambili yake.
  • Baada ya kuumuka weka mayai mawili, kisha changanya mchanganyiko wako vizuri kwa kutumia upawa.
  • Bandika kikaangio chako cha vitumbua jikoni na mchanganyiko upo tayari kwa kuchoma.

Enjoy!!!!!

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s