Asalaam aleikum warahmatullah wabarakatu, natumai swaum zinaendelea salama. Safari hii nimechelewa kupost mapishi ya iftar, kuna baadhi ya mapishi nataka nijaribu, nikiyapatia vizuri In shaa Allah nizipost. Ila kwa sasa hivi ntapost marudio ya mapishi ya ramadhani ya mwaka jana.
Mwenyezimungu abariki funga zetu na apokee swaum zetu. Ramadhan njema.

Mahitaji
- Ndizi mzuzu kilo moja
- Nazi 400ml
- Maji 400ml
- Iliki
Maandalizi
- Menya, kata ndizi zako
- Weka ndizi, nazi 200ml, maji 400ml na iliki kwenye sufuria, kisha bandika jikoni viive.
- Angalia zisiive sana kiasi cha kumong’onyoka. Zikisha iva, zima jiko.
Jinsi ya kutengeneza tui la kupaka
Mahitaji
- Nazi 200ml
- Ngano kijiko kidogo nusu (hii unatumia kama tui lako ni jepesi mno)
Maandalizi
- Chemsha tui lako kwenye kisufuria kidogo. Likianza kuchemka, koroga taratibu hadi liive ili tui lisikatike.
- Tui lako litakuwa tayari kama likiwa zito na linatoa mapovu wakati likichemka.
- Ikiwa tui lako ni jepesi na haliwi zito, changanya ngano na maji vijiko vikubwa vitatu, kisha mimina taratibu kwenye tui lako. Usimimine lote kwa wakati mmoja, likianza kuwa zito, acha lichemke mpk liive.
- Changanya tui lako na ndizi kwa kutumia kijiko. Fanya hivi taratibu kuepusha ndizi kumong’onyoka.
- Ndizi zako tayari kwa kuliwa.
You must be logged in to post a comment.