
Mahitaji
- Ngano 1kg
- Sukari robo (kama weye ni mpenzi wa sukari, unaweza ukaongeza)
- Hamira packet 2 za 7g
- Bakingpowder paket 1 ya 7g
- Nazi au maziwa 1ltr
- Iliki iiyosagwa 2tbs
- Mayai 3
- Mafuta ya kupikia 1ltr
- Makuli kubwa la kukandia
- Karai
- Kibao na msukumio
Maandalizi
- Mimina mafuta kidogo au samli (150ml) kwenye kisufuria kidogo, kisha iweke jikoni yapate moto.
- Mimina unga, sukari na iliki kwenye bakuli la kukandia, kisha vichanganye vizuri
- Mafuta yakishapata moto vizuri mimina kwenye mcchanganyiko wa unga, angalia usiungue.
- Changanya mafuta na unga vizuri, kisha weka hamira na bakingpowder. Changanya vizuri
- Vunja mayai na changanya kwenye mchanganyiko wa unga.
- Mimina nazi au maziwa ya uvuguuvugu taratibu kwenye unga, mpaka upate donge moja. Mchanganyiko usiwe mgumu sana na usiwe chapachapa.
- Kanda ngano yako hadi iumuke.
- Kata madonge tisa. Sukuma kisha kata.
- Bandika Karai lako, weka mafuta, anza kuchoma mahamri yako.
- Yakiwa rangi ya brown, yatoe.
- Mahamri yako tayari kuliwa.
Unaweza kula na mbaazi, maharage au mchuzi.