Jinsi ya kutengeneza ndizi za mzuzu na nazi ya kupaka

Asalaam aleikum warahmatullah wabarakatu, natumai swaum zinaendelea salama. Safari hii nimechelewa kupost mapishi ya iftar, kuna baadhi ya mapishi nataka nijaribu, nikiyapatia vizuri In shaa Allah nizipost. Ila kwa sasa hivi ntapost marudio ya mapishi ya ramadhani ya mwaka jana.

Mwenyezimungu abariki funga zetu na apokee swaum zetu. Ramadhan njema.

Mahitaji

  • Ndizi mzuzu kilo moja
  • Nazi 400ml
  • Maji 400ml
  • Iliki

Maandalizi

  • Menya, kata ndizi zako
  • Weka ndizi, nazi 200ml, maji 400ml na iliki kwenye sufuria, kisha bandika jikoni viive.
  • Angalia zisiive sana kiasi cha kumong’onyoka. Zikisha iva, zima jiko.

Jinsi ya kutengeneza tui la kupaka

Mahitaji

  • Nazi 200ml
  • Ngano kijiko kidogo nusu (hii unatumia kama tui lako ni jepesi mno)


Maandalizi

  • Chemsha tui lako kwenye kisufuria kidogo. Likianza kuchemka, koroga taratibu hadi liive ili tui lisikatike.
  • Tui lako litakuwa tayari kama likiwa zito na linatoa mapovu wakati likichemka.
  • Ikiwa tui lako ni jepesi na haliwi zito, changanya ngano na maji vijiko vikubwa vitatu, kisha mimina taratibu kwenye tui lako. Usimimine lote kwa wakati mmoja, likianza kuwa zito, acha lichemke mpk liive.
  • Changanya tui lako na ndizi kwa kutumia kijiko. Fanya hivi taratibu kuepusha ndizi kumong’onyoka.
  • Ndizi zako tayari kwa kuliwa.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s