Ftari yetu ya leo tunatengeneza chapati za maji za hoho. Chapati zetu zitakuwa za chumvi maana ftari kuu zengine zote nazo ni za chumvi, kwahiyo na chapati zetu tutaweka chumvi. Ila kama unaweza kuchanganya chumvi na sukari, unaweza ukaweka sukari badala ya chumvi, ila hoho sikushauri kuweka kwenye chapati za maji za sukari, utaharibu ladha.

Mahitaji
- Ngano nusu kilo
- Maziwa 300ml
- Maji 200ml
- Hoho nusu
- Chumvi kijiko kidogo nusu
- Mafuta ya kukaangia
Jinsi ya kupika
- Osha hoho, kisha ikate vipande vidogovidogo
- Changanya vitu vyote, kama mchanganyiko mzito sana ongeza maji kidogo.
- Kaanga chapati zako.
You must be logged in to post a comment.