Mishono ya vitambaa

SIku hizi mafundi wa nguo wamekuwa wengi na washonaji hasahasa, ila pia kuna mafundi waharibifu. Mara nyingi tumekuwa tukiona watu wakipost picha instagram za mshono walotaka na jinsi fundi alivyowatolea.

Chanzo cha kuharibiwa nguo na fundi;

 • Material ya kitambaa ulichopeleka sicho cha alichosonea picha ulomuonesha fundi wako
 • Ubahili. Badala ya kuenda kwa fundi unajua atakushonea vizuri, ila kwa kuwa hutaki pesa nyingi upo radhi uende kwa “ibrahim” ambae atakushonea kwa bei rahisi.
 • Tamaa: kuna baadhi ya washonaji wana tamaa sana, badala waseme wazi kwamba huu mshono hawauwezi, wanakubali kukushonea huku wakijua watakuharibia.
 • Maumbile ya mtu: kuna mishono mengine ukiona nguo kavaa mtu mwembamba, mtu mnene/ umbo namba 8 haiwezi kumpendeza na baadhi ya mishono inawapendeza watu wanene/umbo namba 8. Mfano ni nguo yenye mshono wa nguva, mtu mwembamba hampendezi.

Picha zifuatazo ni baadhi ya mishono ya vitambaa aina tofauti tofauti. Kuna vya satin, cotton, chiffon na hata jeans.

Braids

For the past 2 years I’ve been braiding my hair. I used to be a sew-in kinda girl, but that change. It was easy for me since I was so busy with work, then I moved to wigs, even made a fews for myself. Then I did a big chop and I loved it for awhile and in 2019 I got hooked on braids. And since then its been braids braids and more braids, am still learning on how to braid myself, I havent got the grip and the patient… yet.

Anyways, here are a few styles.

Mishono ya vitenge: jumpsuit

Kwenye mada yetu ya leo ya mishono ya vitenge, tunawaletea style ya jumpsuits. Unaweza kushona kwa kutumia kitenge cha aina moja na kuna wengine kutumia vitenge viwili tofauti. Ukitumia vitenge viwili tofauti hakikisha rangi au design zinaendana kidogo.

Kama una mishono ungependa tuweke kwenye blog yetu, usisite kututumia kupitia email au Facebook yetu.

NB: email for credit/removal

Jinsi ya kutengeneza ndizi mzuzu za nazi ya kupaka

Mahitaji

 • Ndizi mzuzu kilo moja
 • Nazi 400ml
 • Maji 400ml
 • Iliki

Maandalizi

 • Menya, kata ndizi zako
 • Weka ndizi, nazi 200ml, maji 400ml na iliki kwenye sufuria, kisha bandika jikoni viive.
 • Angalia zisiive sana kiasi cha kumong’onyoka. Zikisha iva, zima jiko.

Jinsi ya kutengeneza tui la kupaka

Mahitaji

 • Nazi 200ml
 • Ngano kijiko kidogo nusu (hii unatumia kama tui lako ni jepesi mno)


Maandalizi

 • Chemsha tui lako kwenye kisufuria kidogo. Likianza kuchemka, koroga taratibu hadi liive ili tui lisikatike.
 • Tui lako litakuwa tayari kama likiwa zito na linatoa mapovu wakati likichemka.
 • Ikiwa tui lako ni jepesi na haliwi zito, changanya ngano na maji vijiko vikubwa vitatu, kisha mimina taratibu kwenye tui lako. Usimimine lote kwa wakati mmoja, likianza kuwa zito, acha lichemke mpk liive.
 • Changanya tui lako na ndizi kwa kutumia kijiko. Fanya hivi taratibu kuepusha ndizi kumong’onyoka.
 • Ndizi zako tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kutengeneza chapati za maji za hoho

Ftari yetu ya leo tunatengeneza chapati za maji za hoho. Chapati zetu zitakuwa za chumvi maana ftari kuu zengine zote nazo ni za chumvi, kwahiyo na chapati zetu tutaweka chumvi. Ila kama unaweza kuchanganya chumvi na sukari, unaweza ukaweka sukari badala ya chumvi, ila hoho sikushauri kuweka kwenye chapati za maji za sukari, utaharibu ladha.

Mahitaji

 • Ngano nusu kilo
 • Maziwa 300ml
 • Maji 200ml
 • Hoho nusu
 • Chumvi kijiko kidogo nusu
 • Mafuta ya kukaangia

Jinsi ya kupika

 • Osha hoho, kisha ikate vipande vidogovidogo
 • Changanya vitu vyote, kama mchanganyiko mzito sana ongeza maji kidogo.
 • Kaanga chapati zako.