Jinsi ya kutengeneza chapati za maji za hoho

Ftari yetu ya leo tunatengeneza chapati za maji za hoho. Chapati zetu zitakuwa za chumvi maana ftari kuu zengine zote nazo ni za chumvi, kwahiyo na chapati zetu tutaweka chumvi. Ila kama unaweza kuchanganya chumvi na sukari, unaweza ukaweka sukari badala ya chumvi, ila hoho sikushauri kuweka kwenye chapati za maji za sukari, utaharibu ladha.

Mahitaji

 • Ngano nusu kilo
 • Maziwa 300ml
 • Maji 200ml
 • Hoho nusu
 • Chumvi kijiko kidogo nusu
 • Mafuta ya kukaangia

Jinsi ya kupika

 • Osha hoho, kisha ikate vipande vidogovidogo
 • Changanya vitu vyote, kama mchanganyiko mzito sana ongeza maji kidogo.
 • Kaanga chapati zako.

Jinsi ya kutengeneza sambusa

Mahitaji

 • Nyama ya kusaga 1kg
 • Viungo (2tsp turmeric, 1 tbsp ginger powder, 2tbsp paprika powder, 2tbsp curry powder, 2tbsp meat flavour stock)
 • Vitunguu 2-3 vikubwa
 • Hoho 1
 • Thomu iliyosagwa 2tbsp
 • Carrot zilizokwanguliwa 250mg (grated carrots)
 • Manda za sambusa (spring roll pastry)
 • Mafuta ya kukaangia
 • parsley/coriander (dania)
 • Limau 2-3
 • Ngano ya kufungia manda

Jinsi ya kutengeneza

 • Weka mchanyiko wa nyama, viungo, thomu, juice ya limau  kwenye sufuria kubwa. Kisha bandika jikoni.
 • Kataka vitunguu, dania na hoho vipande vidogovidogo na vyembamba. Kisha visafishe, bila kusahau carrot zako. Zichuje vizuri.
 • Usisahau kuigeuza nyama yako. Onja kama imeiva
 • Mimina mchanganyiko wa vitunguu kwenye nyama. Acha ichemke kwa dakika 5-10, kisha onja kama chumvi na viungo vipo sawa. Kama ndogo ongeza. kisha acha ichemke mpaka ukavu maji. Hakikisha imekauka. Kisha zima jiko. Acha ipoe
 • Weka ngano kwenye kibakuli, weka maji, koroga ilikupata mchanganyiko *gundi*
 • Funga manda zako, jaza sambusa. Bonyeza link hapo chini kama hujui jinsi ya kufunga sambusa.
 • Choma sambusa zako. Tayari Kula.
 • Unaweza kuchoma zote au ukahifadhi baadhi kwenye freezer.

How to fold Samosa (2 Ways) By Rubina Asif – YouTube

Jinsi ya kutengeneza ndizi za mzuzu na nazi ya kupaka

Asalaam aleikum warahmatullah wabarakatu, natumai swaum zinaendelea salama. Safari hii nimechelewa kupost mapishi ya iftar, kuna baadhi ya mapishi nataka nijaribu, nikiyapatia vizuri In shaa Allah nizipost. Ila kwa sasa hivi ntapost marudio ya mapishi ya ramadhani ya mwaka jana.

Mwenyezimungu abariki funga zetu na apokee swaum zetu. Ramadhan njema.

Mahitaji

 • Ndizi mzuzu kilo moja
 • Nazi 400ml
 • Maji 400ml
 • Iliki

Maandalizi

 • Menya, kata ndizi zako
 • Weka ndizi, nazi 200ml, maji 400ml na iliki kwenye sufuria, kisha bandika jikoni viive.
 • Angalia zisiive sana kiasi cha kumong’onyoka. Zikisha iva, zima jiko.

Jinsi ya kutengeneza tui la kupaka

Mahitaji

 • Nazi 200ml
 • Ngano kijiko kidogo nusu (hii unatumia kama tui lako ni jepesi mno)


Maandalizi

 • Chemsha tui lako kwenye kisufuria kidogo. Likianza kuchemka, koroga taratibu hadi liive ili tui lisikatike.
 • Tui lako litakuwa tayari kama likiwa zito na linatoa mapovu wakati likichemka.
 • Ikiwa tui lako ni jepesi na haliwi zito, changanya ngano na maji vijiko vikubwa vitatu, kisha mimina taratibu kwenye tui lako. Usimimine lote kwa wakati mmoja, likianza kuwa zito, acha lichemke mpk liive.
 • Changanya tui lako na ndizi kwa kutumia kijiko. Fanya hivi taratibu kuepusha ndizi kumong’onyoka.
 • Ndizi zako tayari kwa kuliwa.

Misuko ya nywele

Nawatakia heri ya mwaka mpya. Nashkuru mwenyezimungu kwa kutuwezesha kuuona mwaka mpya tukiwa wazima na wenye afya. Kwa wale walotangulia mbele za haki, mwenyezimungu awape kaul thabeet na kwa walio wagonjwa tunawaombea na In Shaa Allah mtapona.

Leo nawaletea tena aina ya misuko ya nywele, safari hii ni style ya minyoosho size ya kati. Enjoy!!!

NB: email for credit/removal

Chicken pasta

On today’s what’s for dinner? episode, we are making pasta with chicken.

Marination ingredients

 • 750g boneless chicken
 • 3 lemons
 • 2tbs greek yoghurt (you can use any yoghurt)
 • 1ts paprika powder
 • 1ts garlic powder
 • 1ts ras el hanout
 • 1ts harira

Preparations

 • Cut your chicken in cubes
 • Clean your chicken and drain well
 • Once your chicken is drained, mix the ingredients and let it marinate for atleast 1hr

Ingredients

Preparations

 • Boil your pasta according to the instuctions on de packaging. I changed a thing or two e.g the amount of water + cooking time. I used 3.5L of water and I let it simmer for 20 – 30min. Don’t forget to stir occasionally. Once pasta is done, drain well.
 • Cut your vegetables + mozzarella
 • Add 2tbs of olive oil in a wok pan and wok your vegetables for 3 – 5min. Make sure they are not overdone. You can wok the zucchini separately (they take extra min to be done).
 • Set the vegatables aside
 • Wok your marinated chicken untill their is no water
 • Heat a sausepan with 2tbs of olive oil
 • Add ginger garlic paste, the vegetable you wok and let it simmer for 2 – 3min (medium heat)
 • Add tomato sauce, pesto rosso and let it simmer for 5min on low heat. Sir occationally.
 • Add coconut cream and 400ml water. Let it simmer for 3min
 • Add chicken and the spices
 • Add 1L of water, mozzarella and the grated cheese. Stir carefully and let it simmer for 3 – 5min.
 • Add pasta, stir it well. If its too thick, add more water.
 • Let it simmer on low heat for 5min.
 • Add chopped persely for garnish and your dinner is ready to serve.

Enjoy your meal 🙂