
Mahitaji
- Mchele vikombe viwili (nusu kilo) loweka usiku kucha
- Tui vikombe viwili
- Sukari kikombe kimoja
- Hamira packet moja (kijiko kimoja)
- Iliki kijiko kimoja cha chai
- Mayai mawili
- Mafuta ya kupikia
Maandalizi
- Kikombe utakachotumia kupimia mchele, ndicho utakachopimia sukari na tui.
- Chuja mchele uloloweka vizuri, hakikisha hamna maji yamebakia
- Mimina tui, mchele, sukari, iliki na hamira kwenye blender, chanya mchanganyiki kwa kutumia kijiko ili iwe sawa kisha washa blender lako.
- Saga kwa takriban dakika 10, pumzisha blender lako kila baada ya dakika 2- 3 hii ni kuepusha blender lako lisiungue. Saga hadi uwe laini.
- Angalia uzito ulivyo, kama mzito sana ongeza tui kidogo.
- Weka mchanganyiko wako kwenye bakuli, ufunike na kisha uweke kwenye sehemu yenye joto uumuke . Unaweza uacha uumuke kwa lisaa limoja au mawili au ukiuona ujazo umekuwa marambili yake.
- Baada ya kuumuka weka mayai mawili, kisha changanya mchanganyiko wako vizuri kwa kutumia upawa.
- Bandika kikaangio chako cha vitumbua jikoni na mchanganyiko upo tayari kwa kuchoma.
Enjoy!!!!!

You must be logged in to post a comment.