Mishono ya vitambaa

SIku hizi mafundi wa nguo wamekuwa wengi na washonaji hasahasa, ila pia kuna mafundi waharibifu. Mara nyingi tumekuwa tukiona watu wakipost picha instagram za mshono walotaka na jinsi fundi alivyowatolea.

Chanzo cha kuharibiwa nguo na fundi;

  • Material ya kitambaa ulichopeleka sicho cha alichosonea picha ulomuonesha fundi wako
  • Ubahili. Badala ya kuenda kwa fundi unajua atakushonea vizuri, ila kwa kuwa hutaki pesa nyingi upo radhi uende kwa “ibrahim” ambae atakushonea kwa bei rahisi.
  • Tamaa: kuna baadhi ya washonaji wana tamaa sana, badala waseme wazi kwamba huu mshono hawauwezi, wanakubali kukushonea huku wakijua watakuharibia.
  • Maumbile ya mtu: kuna mishono mengine ukiona nguo kavaa mtu mwembamba, mtu mnene/ umbo namba 8 haiwezi kumpendeza na baadhi ya mishono inawapendeza watu wanene/umbo namba 8. Mfano ni nguo yenye mshono wa nguva, mtu mwembamba hampendezi.

Picha zifuatazo ni baadhi ya mishono ya vitambaa aina tofauti tofauti. Kuna vya satin, cotton, chiffon na hata jeans.